NOS ADRESSES ET CONTACTS

📍 Siège : RDC ; Ville de Goma ; Comme de Goma ; Q. Les Volcans ; Av. Nzumuka James, N°029

Vous ne trouvez pas ? Contactez-nous

samedi, avril 18News That Matters

Goma : Kampeni ya kusaidia wanandoa ao jozi wenye shida ya kupata mtoto

Kuanzia tarehe 19 hadi 22 Januari 2026, Clinique Notre Vie (CLINOVIE), kwa kushirikiana na madaktari wa Nord-Kivu na Université de Goma, linaandaa kampeni maalum ya kusaidia wanandoa wanaopata shida ya kupata mtoto.

Katika kampeni hii, madaktari watasaidia wanandoa ao jozi kuelewa sababu zinazochelewesha kupata mimba, kwa kutumia vipimo vya kisasa na salama vinavyoweza kuangalia hali ya mfuko wa uzazi na njia za mimba kwa mwanamke.

Huduma ao Kazi hizi zitatolewa na madaktari wenye uzoefu ao ujuzi (EXPÉRIENCE), akiwemo Dr Sefu Masamba Polydor, aliyefanya mafunzo yake nje ya nchi, pamoja na madaktari wengine wa Goma.

Waandalizi wa mpango huu (Les organisateurs) wanawahimiza wananchi wa Goma na kandokando hasa wanandoa wanaosumbuliwa na tatizo la kutopata mtoto, kuchukua fursa (OPPORTUNITÉ) hii muhimu, kufika kunako Clinique Notre Vie ili upate ushauri wa kamili, na matibabu inayo faa.

Usibaki na mawazo peke yako.

Kupata maelezo sahihi kunaweza kusaidia kuchukua hatua nzuri kwa maisha ya familia.

📅 Tarehe : 19 – 22 Januari 2026

📍 Mahali : Clinique Notre Vie (CLINOVIE), Goma

📞 Pata rendez-vous :

(+243) 979 525 135 | 895 018 814

Partager

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *